
Mkazi wa jiji la Mbeya ambaye hakufahamika jina lake alikutwa na mpiga picha wetu katikati ya jiji la Mbeya barabara ya Jakaranda akiwasiliana na jamaa zake kwa kutumia simu ambayo alikuwa ameiunganisha na betri za radio,kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba simu yake humsumbua chaji mara kwa mara hivyo analazimika kutembea na betri ikiwa ni njia ya kumrahisishia mawasiliano
(Picha na Rashid Mkwinda)