~ INGEKUWA VIPI KAMA KILA PUMZI UNAYOIVUTA UNGEKUWA UNAILIPIA??~
Tuesday, March 04, 2008
Mtoto anapozaa watoto
Msichana huyu ana bahati mbaya ya maisha yake amezaliwa miaka 14 iliyopita, mzazi wake alimtupa katika rambo, akaokotwa na wasamaria wema huko Makete mkoani Iringa na kulelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Bulongwa aliondoka na kufika katika mji mdogo wa Tunduma akiwa na umri wa miaka 13 bahati mbaya alidanganywa na mpiga debe na kumpachika mimba na kuzaa watoto mapacha,mpiga debe kamtelekeza hivi sasa anahaha mitaani akiomba msaada kwa wasamaria wema, Maskini binti huyu!!!!!!
(Picha na maelezo kwa hisani ya rashid Mkwinda)
 
© Rama Msangi |Tarehe: 11:14 AM | Permalink |


Maoni: 4


  • Tarehe: May 3, 2008 at 9:08 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    ..jamani mie nimeguswa sana lakini kwa sasa sipo tz..ila nilikuwa natoa ushauri wewe kama blogger umwambie huyu binti aende ustawi wa jamii.watamsaidia..kwasababu ni jukumu lao..hao watoto wasipate shida kwani ni wadigo sana..na huyu binti aweze kurudi shule.

     
  • Tarehe: September 3, 2008 at 12:33 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    mambo vipi mkuu?
    Nahitaji email yako ninataka kuwasiliana na wewe
    muhimu mzee we iweke hewani hapa nitakutumia mail

     
  • Tarehe: September 27, 2008 at 4:02 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Hapa ndipo ninapoona umuhimu wa mila za jando na unyago. Kipindi cha mila ile watu walijitambua na kutambua wenzao. Katika hili hata wanyama wana ustaarabu na ni unyama zaidi ya wanyama kumzalisha binti mwenye umri kama huo. Huyu amebahatika japo kuripotiwa katika blogu je wengine wanaoishia kubakwa kila siku kwa ajili ya kulipa gharama za malezi yao? Siku kiama kitakaposimama sijui tutatokea wapi.. Eee mola tunusuru!

     
  • Tarehe: October 4, 2008 at 3:01 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Rama Msangi

    kwa wale wenye kuhitaji email yangu ni msangirs@gmail.com