~ INGEKUWA VIPI KAMA KILA PUMZI UNAYOIVUTA UNGEKUWA UNAILIPIA??~
Saturday, February 09, 2008
Soma kilichomng'oa Lowasa madarakani
kwa marefu na mapana, naomba wasomaji wangu mpate fursa ya kupitia kitu kipya leo ambacho loicha ya kuwa si picha, lakini kimeleta picha mpya katika historia ya taifa la Tanzania. Namaanisha ripoti kuhusu Kashfa ya Kampuni hewa ya kuzalisha Umeme iitwayo Richmond. Ripoti hiyo iliwasilishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katikati ya wiki linaloelekea ukingoni, na kusababisha kishindo kikubwa sana katika medani za siasa za Tanzania.

Najua si wote mliiona ripoti hiyo ilipokuwa ikiwasilishwa Bungeni, na si wote mliosikia, na pia si wote mmeweza kuipata. Sasa kwa wale ambao hawakubahatika kote huko, naomba muipitia kwa kubonyeza hapa.
 
© Rama Msangi |Tarehe: 10:35 AM | Permalink |


Maoni: 0