~ INGEKUWA VIPI KAMA KILA PUMZI UNAYOIVUTA UNGEKUWA UNAILIPIA??~
Monday, February 04, 2008
Ni gereji au duka la vyuma chakavu?
Tunduma sio tu imekuwa sehemu yenye kukera kutokana na foleni za kijinga sana ambazo zinatokana na uzembe wa maafisa wa pale mpakani. Fikiria tulikaa na maiti katika foleni kwa karibu saa mbili unusu? Lakini si hayo tu, tizama na huu uchafu unaoonekana hapo pichani ambao eti tuliambiwa sehemu hiyo ni gereji. Gereji!! hivi tunazijua gereji au tunataniana wajameni!!
 
© Rama Msangi |Tarehe: 10:39 AM | Permalink |


Maoni: 0