~ INGEKUWA VIPI KAMA KILA PUMZI UNAYOIVUTA UNGEKUWA UNAILIPIA??~
Monday, December 31, 2007
Usishangilie kama hujauona live bwana....ohooo
Aisee, kama hujauona rasmi mwaka mpya, basi usijisifu na kuanza kuupangia mipango. Jamaa waliokuwa kwenye kipanya hapo chini huenda walishaanza na kuusherehekea, lakini dereva mmoja mzembe akawakatisha maisha yao saa chache sana kabla hawajaiona 2008
Jamaa aliyekuwa akiendesha kipanya hicho alishindwa kuimudu kona unayoiona upande wa kulia mwa picha, na kilichofuatia alilivaa lori lililokuwa limesimama kando ya barabara. Lori hilo pichani chini, lilikuwa limebeba ulanzi (Maggid nadhani anaielewa vizuri hii kitu), na miongoni mwa raia wanne waliopoteza maisha katika ajali hiyo, wapo waliokuwa wakikinga pombe hiyo kwa ajili ya kuanza kuichuuza
Hapa chini ni mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo, ambaye walau yeye atauona mwaka 2008, ingawa atakuwa yuko kitandani katika moja ya hospitali za jijini Mbeya.
Ajali hii ilitokea eneo la Uyole ya Kati, katika jiji la Mbeya (Picha kwa hisani ya Rashid Mkwinda)
 
© Rama Msangi |Tarehe: 1:10 PM | Permalink |


Maoni: 0