Mji wa Tunduma ni mji maarufu sana nchini, uko mpakani mwa Tanzania na Zambia na kwa hakika ni mji ambao uko busy kupita maelezo, unaweza kuona picha hapa uone jinsi ambavyo pilika pilika ziko nyingi katika eneo hilo

 Wingi wa watu, magari, majengo na rabsha zingine za kimjini, ni iongoni mwa mambo ambayo katika mazingira ya kawaida, ungetarajia yawaamshe wale wanaohusika na usimamizi wa mji huo, kusudi waandae plani nzuri ya kuuimarisha na kuuboresha....lakini jamaa wako kimya.

 Pilika pilika zinazidi kuongezeka siku hadi siku, lakini hakuna mkakati wa kuboresha mfumo wa mpangilio wa mji huo. Najiuliza hivi hawa jamaa wanasubiri hali iwe mbaya ndio waanze kuwabomolea watu au?
Picha kwa hisani ya Rashid Mkwinda