~ INGEKUWA VIPI KAMA KILA PUMZI UNAYOIVUTA UNGEKUWA UNAILIPIA??~
Friday, December 07, 2007
Tiba za asili

Kuna maswali kadhaa najiuliza kuhusu hawa jamaa zetu. Ni kweli kuwa wanaume wamekuwa na shida sana ya kuongeza nguvu zao? Maana kila kona ukipita ni dawa za kuongeza nguvu za kiume? Kuna tatizo gani hasa hapo?
 
© Rama Msangi |Tarehe: 11:48 AM | Permalink |


Maoni: 1


  • Tarehe: January 18, 2008 at 3:29 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Nasikitika kuona una swali juu ya hili. Ok labda hukuwa unajua, lakini ukweli ni kwamba idadi ya wanaume wenye kusumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume ni kubwa mno. Ni kwa sababu ya aina ya vyakula wanavyokula, kemikali ni nyingim tofauti na walivyokuwa wazee wetu.

    Inaonekana bado ni kijana sana, pengine huwa hufanyi tafiti, lakini huu ndio ukweli. Ni hoja nzuri hiyo, lakini ungeanzisha kwa Serikali kuangalia uwezekano wa kushirikiana na watu hawa, yawezekana kweli wana dawa, lakini yawezekana pia wengine wasanii, nani ajuaye.

    Kama ambavyo dawa za asili za kichina zina nguvu duniani, kuna haja ya kuhakikisha waganga wa asili wanakusanywa kisha kusaidiwa ili tiba zao ziweze kuwa za kisasa na hata zikauzwa nje.

    Binafsi nina amini tiba asili kuliko za kisasa, wakati fulani japo ni mwandishi wa habari, lakini huwa nashirikiana na wataalam wa kisasa hasa Muhimbili, kufanya utafiti kuhusu tiba asili, mfano hivi karibuni tulikuwa tunachunguza haba soda, dawa ambayo imezungumzwa sana kwenye vitabu vya kiislam, kiasi kwamba kwenye kitabu fulani, niliona imeandikwa kuwa hakuna ugonjwa usiotibika na haba soda.

    Tiba asili zipo. babu zetu walikuwa wakitumia hizo na walikuwa na afya njema na kuishi miaka mingi, shida ni kwamba siku hizi wengi wasanii...kiasi kwamba inakuwa vigumu kujua nani mkweli nani mwongo. Ila tiba asili ni nzuri zaidi kuliko za kisasa, utaona vitu kama mbinu za mapapai ni tiba nzuri kabisa kwa malaria, mbegu za mbuyu nazo ni tiba nzuri kabisa kwa wale wenye tatizo la nguvu za kiume, kama utakumbuka ndiyo iliwahi kupigiwa kelele bungeni kwamba kuna jamaa alitumia nguvu zikawa mara dufu....

    kama ambavyo watu wanatumia majani ya mirungi na kulewa, iko mimea ni tiba, ina vitamini na madini fulani...swali ni je kweli wote wanaouza tiba za asili wana utaalam? NO.