
 Pichani ni mwandishi Rashid Mkwinda, akiongea na mmoja wa walemavu walioko katika mji wa Dodoma, kuhusiana na anavyoendesha maisha yake. Mlemavu huyo wa miguu na mikono anasema 'anatembea' zaidi ya kilomita 4 kila siku kufika mjini kusudi aombe wasamaria wampatie chochote kwa ajili ya kuendesha maisha yake. 
Hivi tuna mpango mkakati wa kuwasaidia walemavu wa aina hii hapa nchini?