~ INGEKUWA VIPI KAMA KILA PUMZI UNAYOIVUTA UNGEKUWA UNAILIPIA??~
Friday, December 07, 2007
Ndoto inataka kuwa kweli?
Jitihada za kuuboresha mji wa Dodoma katika miaka ya karibuni zimekuwa kubwa sana. Au wakubwa baada ya longolongo za muda mrefu bado wana ile ndoto ya kuhamishia makao makuu katika mji huo? Pichani ni sehemu ambayo zamaaaaaaani sana ilikuwa na soko likabomolewa na sasa watengeneza bustani, au tuseme sehemu ya kupungia upepo na ina mnara wa hayati Baba wa Taifa, Mwl JKN.

Picha ya chini, ni moja ya mabango yanayoupendezesha mji huo, kama nilivyokumbana nalo katika sehemu hiyo hiyo ya kupumzikia, al maarufu kwa jina la Nyerere Square. Hivi tunamuenzi kweli lakini?

 
© Rama Msangi |Tarehe: 12:05 PM | Permalink |


Maoni: 0