~ INGEKUWA VIPI KAMA KILA PUMZI UNAYOIVUTA UNGEKUWA UNAILIPIA??~
Monday, December 31, 2007
Mikakati miiiiiingi, ajali nazo nyiiiiiingi... kwanini...Why!!
Mikutano ya kuhamasisha masuala ya usalama ukiwemo wa barabarani imekuwa ikiitishwa mara kwa mara katika miaka ya karibuni ili kujitahidi kuepukana na ongezeko la ajali hizi. Kama hapa ambapo kamanda wa polisi mkoani Mbeya Bw. Suleiman Kova, alipokuwa akiongea na wananchi wa mji mdogo wa Tunduma


Kizuri zaidi ni kuwa mikutano ya namna hii imekuwa ikigharimu fedha nyingi sana kuiitisha ikiwa ni pamoja na kuweka mambo ya burudani kusudi watu wahamasike kujitokeza na kusikiliza neno hilo la uzima


Cha ajabu sasa ni kuwa kwa kadiri juhidi hizo zinafanyika, ndivyo ambavyo ajali nazo zimekuwa zikiongezeka. Tatizo niniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!! eeh wanaume....why??

 
© Rama Msangi |Tarehe: 12:15 PM | Permalink |


Maoni: 0