~ INGEKUWA VIPI KAMA KILA PUMZI UNAYOIVUTA UNGEKUWA UNAILIPIA??~
Friday, December 07, 2007
Maggid, Ndesanjo, Jeff...nani alidensi NK?
Sijui nani ambaye enzi zake aliwahi kuserebuka katika jumba la NK lililoko maeneo ya Jamatini, mjini Dodoma. Sikuwa mpenzi sana wa dansi (kwakuwa miziki mingi ya enzi zile ilibidi mtu uwe una utaalamu wa yoga), lakini mara moja moja nilikuwa mtazamaji. Jumba hilo bado linadunda hadi leo, ila sasa kila ukikatiza hapo ni huu muziki wa kizazi kipya. Mliowahi kucheza dansi hapo mlie tu, zama zenu zimeondoka na nyie

Ila jengo hili la CCM makao makuu lingali linadunda bwana. Hapa ndipo yalipo makao makuu ya Chama kinachoshikilia utamu wa nchi hii............. aluuuu....we acha tu
 
© Rama Msangi |Tarehe: 12:13 PM | Permalink |


Maoni: 0