~ INGEKUWA VIPI KAMA KILA PUMZI UNAYOIVUTA UNGEKUWA UNAILIPIA??~
Monday, December 31, 2007
Kitu gani kimelikumba vazi hili jamaniiiiiiii!!!!
Inaniumiza kichwa na imeniumiza kwa muda mrefu sana kwakweli. sasa naomba mnisaidie. Zamani, enzi hizo, miaka hiyo, kipindi hicho, miaka hiyo ya nyuma, hili vazi analolinadi jamaa, lilikuwa vazi ambalo usingetarajia kuwa liwe namna hii. Lilikuwa vazi ambalo hata ukienda dukani kununua unasubiri watu wengine watoke ndio uagize haraka haraka kabla hajaibuka mteja mwingine akajua unanunua nini.

kufua kwake ndio usiseme. Lilikuwa linafuliwa katika eneo maalum, na kuanikwa sehemu ya kipekee (mie ilikuwa chini ya godoro, wewe je), lakini sasa mh!!!

Mambo ndio kama haya. Linapitishwa mitaani kama karanga vile. Ukikatiza kitaa ya uswahilini huko, unakuta watu wanafua hata upenuni mwa nyumba zao, achilia mbali kuanika hata kandokando ya barabara.
Ni utandawazi au ni kuwa limeanza kushuka hadhi yake!! Kitu gani hasa kimelikumba vazi hili?
Picha kwa hisani ya Mkwinda
 
© Rama Msangi |Tarehe: 2:01 PM | Permalink |


Maoni: 3


  • Tarehe: December 31, 2007 at 2:33 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Hayo ndio matoke ya utandawazi,kama baadhi ya wavaaji wa vazi ilo wanashindwa kulisitiri vizuri maungoni mwao unategemea wauzaji wafanye nini zaidi ya kulinadi utafikiri samaki feri!!!

     
  • Tarehe: January 1, 2008 at 2:42 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    AISEE...halafu siku hizi yaani unakuta mtu anakatiza mbele yako au mbele yenu kashikilia hicho kivazi, kisha anaanza kuvuta na lastiki kabisa uhu akisema "tizama braza/sista...hii inakutosha kabisa"

    zamani bwana ilikuwa ukiingia dukani kununua kwanza unasubiri watu watoke wote kisha unaagiza haraka haraka tena ile unayoiona mbele yako, na kuondoka haraka haraka ili watu wasikukute hapo....ndio maana nyingine zilikuwa zinakuwa kuuuubwa ama zingine ndooogo....

    mh!!!

     
  • Tarehe: January 1, 2008 at 1:55 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Rashid Mkwinda

    Nilichokiona na mambo ya mwaka mpya 2008!!!!!!! hadi raja Big up Maan!! badilisha jina sio Msangi Mdogo sasa nadhani umekwisha kuwa Msangi mkubwa hivi wewe ukiwa Msangi Mdogo, mwanao Said naye ataitwa nani?ulikuwa mdogo enzi zile sio sasa juzi juzi tu ulikuwa ni Baba wa Bwana harusi kule Dom bado ni Msangi mdogo tu!!!! badilika Maaaan!!!! but bg up