~ INGEKUWA VIPI KAMA KILA PUMZI UNAYOIVUTA UNGEKUWA UNAILIPIA??~
Friday, December 07, 2007
Hebu fanya hivi......
Tazama hiyo picha uzuri, nadhani wengi mtakuwa mnakumbuka kuwa yalikuwa yale mabango ambayo yalisambazwa enzi za kampeni, wakati JK anawania kuingia magogoni pale. Sasa hebu fanya hivi, angalia uzuri ile kauli mbiu ya jamaa, kisha chukua herufi moja ya kwanza kabisa katika ule mstari wa kwanza ambayo ni A. Baada ya hapo chukua herufi tatu za mwanzo katika mstari wa pili ambazo ni NGU, halafu chukua herufi mbili tu za mwanzo katika mstari wa tatu ambazo ni KA.

Ukiziunganisha unapata neno gani mwanawane? Na je, zinaleta maana kwa kuangalia uhalisia wa hali ilivyo sasa au ni uzushi wangu tu? Tuko katika mwelekeo wa kauli mbiu hiyo au tuko katika mwelekeo wa kifupisho cha kaulimbiu hiyo?
 
© Rama Msangi |Tarehe: 12:24 PM | Permalink |


Maoni: 1


  • Tarehe: December 7, 2007 at 9:09 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Rama,
    Hongera kwa jicho hili la tatu.Ulichokiona na kutuonyesha kina mantiki.Kazi kweli kweli.Kwa mwendo huu wa kuanguka basi tumekwisha au tunajimaliza?