Tizama hiyo picha, tizama hiyo hundi anayokabidhiwa JK, tizama kiasi cha pesa kilichoandikwa katika hundi hiyo. Hebu kitizame tena kiasi kilichoandikwa kwenye hundi hiyo, kile kilichoandikwa kwa maneno, na kile kilichoandikwa kwa tarakimu. Ama!! Hivi "two hundred thousand" ni sawa na 300,000,= kweli? JK, hivi uliliona hilo lakini? sio changa la macho hilo? hapana, kuna walakini hapa!!
Picha hii ni kwa hisani ya mtandao wa gazeti la Majira, na maelezo ya picha hiyo katika gazeti la majira la leo, sanjari na kule kwenye mtandao nilipokutana nayo yalikuwa haya yafuatayo:-
araJamani hii ni aibu na hivi nadhani ndivyo tunavyodanganywa kila wakati, lakini hebu na tuangalie inawezekana jamaa kachukua cha juu akasahau kuweka vizuri tarakimu zake, utadhani ni mambo ya kusadikika kumbe ni vi2 halisi kabisa, jamani fedheha hii hadi lini? hadi Rais wetu anadanganywa ina maana....du nashindwa hata kusema...hiii coment nadhani hii ni coment ya mwaka binafsi nakupa tuzo kwani inaonekana ni wazi kuwa jicho lako la tatu linafanya kazi